Orkonerei FM

Changamoto za ankara za maji Terrat: Bili kubwa kuliko matumizi

17 October 2025, 10:57 am

Mwanamke akijaza ndoo kwa maji ya bomba (Picha na shirika la EPA/LEGNAN KOULA.)

Kurunzi Maalum

Orkonerei FM Radio kupitia kipindi cha Kurunzi Maalumu inamulika sekta ya maji, ikizungumzia changamoto za bili (ankara) za maji katika Kata ya Terati, Wananchi wengi wanalalamika kupokea bili zinazokuja na gharama kubwa, na wakati mwingine wanaona ni kubwa zaidi ya matumizi halisi.

Kipindi hiki kimeongea na wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Terati, na mamlaka husika kueleza mzizi wa tatizo na jinsi ya kuripoti changamoto zilizopo.

Makala ya Kurunzi maalum Ijumaa Tarehe 17 Oktoba 2025 Saa 08:30 Asubuhi