Orkonerei FM

Wahanga wa bili kubwa za maji Terrat waeleza changamoto

17 October 2025, 8:18 am

Na Isack Dickson

Wakazi wa Kijiji cha Terrat, Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wanakabiliwa na changamoto ya kupokea bili za maji ambazo hazilingani na matumizi yao halisi, huku wakidai kuwa bei hizo ni kubwa na zinawatesa.

Baadhi yao wanasema kuwa bili inakuwa kubwa kupita kiasi, ambapo mmoja alidai kudaiwa shilingi laki moja na sitini na tano elfu huku akitumia kiasi kidogo tu.