Orkonerei FM
Orkonerei FM
3 October 2025, 12:19 pm

Na Dorcas Charles-Kurunzi Maalum
Idadi ndogo ya vijana wa kike kutoka jamii za kifugaji katika Wilaya ya Simanjiro wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi inazua maswali mengi juu ya ushiriki wa wanawake vijana katika siasa. Hali hii inajiri wakati nchi ikiendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika Kurunzi Maalum (Kipindi) kinachorushwa na Orkonerei FM Radio, kiliangazia changamoto na fursa zinazowakabili vijana hawa. Dorcas Charles, mtangazaji wa makala hii, alieleza kuwa vikwazo vikuu ni pamoja na mila na desturi za jamii, majukumu ya kifamilia na ukosefu wa elimu ya uraia.
Licha ya takwimu za mwaka 2020 kuonesha asilimia ndogo ya wanawake vijana waliojitokeza kugombea, bado kuna matumaini. Jamii na serikali zina jukumu la kuhakikisha vijana hawa wanapata fursa sawa na usawa wa kijinsia unaimarishwa katika michakato yote ya kidemokrasia.
Sikiliza kipindi kizima cha “Kurunzi” ili kupata maelezo zaidi juu ya mada hii muhimu.