Orkonerei FM
Orkonerei FM
1 October 2025, 4:10 pm

Na Dorcas Charles
Kila Septemba 28, dunia huadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani ili kutoa elimu juu ya madhara ya ugonjwa huu na namna unavyoweza kuzuilika. Afisa Mifugo wa Kata ya Terrat, Petro Mejooli Lukumay, amesema chanjo ya mbwa ndiyo kinga pekee kwani ugonjwa huu hauna tiba. Amehimiza jamii kuhakikisha mbwa wanachanjwa kila mwaka na kuchukua hatua za haraka endapo mtu atang’atwa.