Orkonerei FM

Unafanya nini kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia?

5 July 2025, 9:14 am

picha kw msaada wa mtandao

Tanzania ina sera na sheria mbalimbali zinazopinga ukatili wa kijinsia, ikiwemo Sheria ya Makosa ya

Kujamiiana ya mwaka 1998, inayolinda hasa wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili

Na pia ipo Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16, ambayo inaweka wazi kuwa ukatili wa aina yoyote ile ni kosa la jinai na adhabu yake inaweza kufikia kifungo cha muda mrefu jela.

Hata hivyo, changamoto kubwa ni kwamba bado kuna watu ambao hawatoi taarifa sahihi kwa vyombo husika kutokana na sababu mbalimbali kama woga, muhali, au kutokujua wapi pa kwenda.

Na hapa ndipo umuhimu wa elimu ya sheria na haki za binadamu unapoonekana dhahiri. Ili kupata picha kamili, sasa tuwasikilize wananchi wa Engonongoi wakijadili kwa kina namna wanavyoripoti matukio ya ukatili wa kijinsia

mjadala mzito kutoka kwa wananchi hawa. Inaonekana wazi bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika kuhamasisha jamii kuripoti matukio haya rasmi ili hatua sahihi zichukuliwe.