“Kilichotokea ni mauaji, inaelezwa kwamba walikuwa baa, baada ya kuwa baa nadhani ugomvi ulitokea, wakapigana. Akachukuliwa akaenda kufia hospitalini. Vijana wengine kutoka kule anakotoka marehemu walikuja kuchoma moto nyumba ya mtuhumiwa na kuharibu migomba iliyokuwa karibu na nyumba hiyo,” amesema Lemeitei.
Na Nyangusi Ole Sang’ida
ijana mmoja aitwaye Joseph Gadiel mkazi wa kitongoji cha Kimelok, kijiji cha Ngiresi wilayani Arusha ameuawa kwa kuchomwa kisu baada ya kutokea ugomvi baina yake na kijana mwingine aliyetambulika kwa jina la William Mungas Sandile, mkazi wa kitongoji cha Olturoto.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji cha Ngiresi, Jonas Lemeitei amesema tukio hilo limetokea baada ya vijana hao kutokea kwenye baa ambapo ugomvi uliibuka na kupelekea Joseph kuchomwa kisu na kufariki dunia alipofikishwa hospitalini kwa matibabu.
Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji
Ameongeza kuwa tayari tukio hilo limeripotiwa Polisi, na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ugomvi huo.
Kwa upande wake, Aminiel Simon, mkazi wa Olturoto, amesema alishuhudia tukio hilo na kwamba vijana hao wenye hasira walikuwa wakitafuta kumdhuru mtuhumiwa lakini walipomkosa wakaamua kuchoma nyumba yake.
Sauti ya Shuda
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha bado hajatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili. Polisi wanaendelea kumsaka mtuhumiwa ambaye ametoroka baada ya kufanya tukio hilo.
Wananchi wametakiwa kuwa watulivu na kuacha kujichukulia sheria mikononi, badala yake kuruhusu vyombo husika kuchukua hatua za kisheria.