Orkonerei FM

Nini Kifanyike Watu Wenye Ulemavu Kuwania Nafasi za Uongozi?

10 April 2025, 10:34 am

Nijuze Radio Show

Katika toleo hili la Nijuze Radio Show, timu ya Orkonerei FM inarushia matangazo moja kwa moja kutoka Kijiji cha Naisinyai, Simanjiro. Dorcas Charles na Isack Dickson wanakutana na wakazi wa eneo hilo, viongozi wa kijamii, watu wenye ulemavu, na Diwani wa Viti Maalum kujadili kwa pamoja namna watu wenye ulemavu wanaweza kujiamini na kushiriki kwenye nafasi za uongozi, hususan wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Kipindi kinazungumzia changamoto zinazowazuia watu wenye ulemavu kushiriki uongozi kama vile mitazamo hasi, mazingira yasiyo rafiki, unyanyapaa, na ukosefu wa ushirikiano na hatua ambazo jamii inapaswa kuchukua kuwawezesha. Pia kunapatikana simulizi za mafanikio ya vijana wenye ulemavu walioanza kujitokeza kwenye harakati za uongozi, mjadala wa wazi chini ya mti na wananchi, pamoja na mahojiano maalum na Afisa Ustawi wa Jamii.