Orkonerei FM

Kituo cha afya Mererani chakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba, miundombinu

4 January 2025, 12:52 pm

Kituo cha afya Mererani picha na mwandishi wetu Joyce Elius

Kituo cha afya  Mererani kilichopo mkoa wa Manyara wilaya Simanyiro bado kinakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwamo vifaa tiba, majengo na miundombinu mingine.

Hayo ya mebainishwa na Dkt. Namnyak Jackson Lukumay wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa Orkonerei Radio. Mwaka 2023 tulizungumza na mtaalam huyu wa afya, viongozi wa kijamii pamoja na wananchi wa eneo hilo na walibainisha changamoto hizohizo na kwamba bado hazijatatuliwa

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Endiamtu  Bw. Sulemani Twaha amesema wanaendela kupaza sauti bila kuona matokeo yoyote katika kitu hicho cha afya.

Sauti ya Suleman Twaha

Kwa upanda wa wananchi Abdallah Ally Nango na Esther Peter nao wamezungumzia hizo changamoto zinazokabili kituo cha afya Mererani

Sauti ya Abdalla Ally
Sauti ya Ester Peter