Orkonerei FM

Unafanya Nini Mwanamke Kushiriki Kuwania Nafasi za Uongozi?

24 October 2024, 11:30 am

Nengai Makaro mwenyekiti wa kitongoji cha Olosira Kijiji cha Lorokare kata ya Oljoro No.5 Wilaya ya Simanjiro ambaye ndiye mwanamama pekee mwenyekiti wa kitongoji kwa Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara. (Picha na Evanda Barnaba).

Nijuze radio Show

Katika toleo hili la Nijuze Radio Show, Orkonerei FM inazunguka moja kwa moja hadi Kijiji cha Lorokare, Kata ya Oljoro No. 5, kuangazia nafasi ya mwanamke katika uongozi na changamoto zinazoikabili jamii ya Kimaasai katika kuwahusisha wanawake kwenye maamuzi na siasa.

Dorcas Charles na Isack Dickson wanazungumza na wananchi, viongozi wa kijiji, wazee wa kimila, na wanawake ambao wamewahi kugombea au kushika madaraka. Kupitia simulizi halisi, mjadala wa wazi, na maoni ya wasikilizaji, kipindi kinaibua changamoto kama mila kandamizi, tamaduni zisizowapa wanawake nafasi, ukosefu wa kujiamini, na mfumo dume unaowakwamisha wengi.

Kipindi pia kinatoa mifano hai ya wanawake waliothubutu kama mwenyekiti wa kitongoji aliyeshinda nafasi hiyo na maoni ya Laigwanani kuhusu nafasi ya mila kubadilika ili kumruhusu mwanamke kushiriki uongozi.