Orkonerei FM

Ikolojia ya Simanjiro Lolkisale waaga watumishi wawili

14 September 2024, 7:07 pm

Baadhi ya watumishi wa TAWA Ikolojia ya Simanjiro Lolkisale,viongozi wa serikali na wananchi katika picha ya pamoja kwenye hafla ya kuwaaga watumishi waliomaliza muda wao wa kutumikia Ofisi hiyo. (picha na Fransisca Fabiana)

Na Joyce Elius na Grace Nyaki

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ofisi ya kamanda mfumo wa Ikolojia Simanjiro Lolkisale iliyopo Terrat imefanya hafla ya kuwaaga watumishi wawili waliokuwa wakitumikia kituo hicho.

Katika sherehe hiyo iliyoahudhuriwa na wananchi, watumishi wa serikali na viongozi mbalimbali wa kisiasa, dini na kimila imefanyika siku ya Tar.13 Septemba 2024 ikishuhudia wastaafu hao wakipokea pongezi na zawadi kutoka kwa watu mbalimbali.

Wakizungumza katika hafla hiyo afisa tarafa wa Tarafa ya Terrat ndg Lekishon Kiruswa,Diwani wa kata ya Terrat Ndg.Jackson Materi,katibu mwenezi wa CCM Terrat Ndg,Lazaro Oltimbau na  Alaigwanani Lesira Samburi wamewasema kuwa watumishi hao wametumikia kwa uweledi na kutoa ushirikiano bora kwa wanajamii.

Kwa upande wa wastaafu Japhet Mungure na Johnson Anangira wamesimulia safari yao ya utumishi ilivyojaa na maswahibu mbalimbali.