Madhila kwa wanawake Lorokare wakitafuta maji
3 September 2024, 4:32 pm
Kijiji cha Lorokare kata ya Oljoro No.5 wilaya ya Simanjiro wanafukua korongo la msimu ili kupata maji ya kutumia kwa shughuli zote za kibinadamu. Ikiwa utahitaji maji safi ya kunywa kutoka bombani basi itakulazimu kutembea umbali mrefu zaidi ya Km 10 kutoka kitongoji cha Songambele hadi Kampuni.
Wanawake katika kijiji hicho wanaendelea kupata mateso ya kifamilia ikiwa ni pamoja na kupigwa na waume zao kutokana na kutumia muda mrefu kutafuta maji.
Diwani wa kata ya Oljoro No.5 Mh. Loshiye Lesakui ameeleza mikakati waliyonayo katika kutatua kero ya upatikanaji wa maji katika kijiji cha Lorokare.
Kipindi cha mvua za masika katika maeneo ya Simanjiro ni kuanzia mwezi Februari kwenda hadi April na kipindi cha kiangazi kuanzia mwezi Julai hadi Novemba.