Orkonerei FM

Justdiggit wazindua Kijani App kwa ajili ya Wakulima

9 August 2024, 1:24 pm

Kijani App kuwezesha wakulima kupata taarifa sasa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Picha kwa hisani ya Shirika la Justdiggit.

Shirika lisilo la kiserikali la Justdiggit limezindua rasmi programu inayofahamika kama Kijani App ili kuwasaidia wakulima kupata taarifa sahihi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi katika kutekeleza shughuli zao za kilimo ili kujiletea maendeleo.

Na Baraka David Ole Maika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Justdiggit kwenye maonesho ya wakulima Nanenane jijini Dodoma Meneja Uhuishaji Ardhi wa Shirika la Justdiggit Mary Sengelela amesema kuwa wanafanya kazi ya kukijanisha mazingira ili kufikia azima na dhamira yao ya kupooza dunia pamoja na kutoa semina kwa wakulima ya jinsi ya kupakua na kutumia programu hiyo ya kijani.

Sauti ya Mary Sengeleka Meneja Uhuishaji Ardhi wa Shirika la Justdiggit

Naye mmoja wa wakulima mnufaika wa programu ya kijani ya shirika la Justdiggit Bw. Ivan John Lugwa kutoka kijiji cha Mkamantwa amebainisha furaha walionayo na jinsi walivyonufaika baada ya kuletewa programu ya kijani na Shirika la Justdiggit.

Sauti ya mkuliwa wa kijiji cha Mkamantwa Bw. Ivan John Lugwa.

Shirika la Justdiggit ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na shughuli za ukijanishani na kutoa usaidizi wa taarifa sahihi kwa wakulima kupitia programu inayoitwa Kijani App.