Orkonerei FM

Maendeleo ya miundombinu Kata ya Terrati Simanjiro Mkoani Manyara

30 July 2024, 3:34 pm

Diwani wa Kata ya Terrat bwana Jackson Materi

picha na Isack Dickson

Na Evanda Barnaba

Ujenzi wa Barabara ya kuunganisha vijiji vya Terrat,Loswaki na Engonongoi bado unaendelea kusubiri mfumo wa serikali unaohusisha kutolewa kwa fedha mara baada ya mwaka wa fedha kuanza mwezi julai mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Diwani wa kata ya Terrat ndg Jackson Matery wakati akizungumza na orkonerei fm Radio,ambapo amesema ahadi yake aliyoahidi mwezi mmoja uliyopita bado ipo na kwamba ujenzi wa Barabara hiyo utakamilika Pamoja na madaraja kwa wakati.

Kuhusu soko la loswaki kutokuendelea ,Diwani Materi amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaotaka madaraka na sio maendeleo na wanaodhoofisha maendeleo ya soko hilo.

Kwa upande mwingine Mh.Matery amesema kuwa amewaka mkakati wa kuunganisha vijiji vyote na atahakikisha zinajengwa stendi katika vijiji vyote vitatu vya kata ya teraat ili kurahisisha usafiri,usafirishaji na biashara.

Sauti ya diwani wa kata ya Terrat Jackson Matery