Orkonerei FM

Mbinu bora za uhifadhi mazao ya chakula

24 July 2024, 2:37 pm

Picha kwa msaada wa mtandao

Na Evanda Barnaba

Uhifadhi wa mazao ya chakula ni suala muhimu sana, hasa kwa wakulima na jamii zetu kwa ujumla. Mazao mengi yanaharibika baada ya mavuno kutokana na uhifadhi duni, jambo ambalo linaweza kusababisha upungufu wa chakula na hasara kubwa kwa wakulima.

Jamii na wakulima hawana uelewa wa namna bora ya kuhifadhi mazao ya chakula, na hii ikanifanya awali kumtembelea mkulima bwana maulidi hashimu kutoka kijiji cha loksale kuzungumza naye mchakato mzima kuanzia anavyoanza maandalizi ya kilimo mpaka kuvuna na namana ambavyo yeye anahifadhi mazao yake ya chakula

karibu kusikiliza makala hii ya kurunzi ili kujifunza mbinu mbalimbali za uhifadhi bora wa mazao ili kusaidia kuhifadhi mazao yetu kwa muda mrefu.