Maadhimisho ya siku mazingira duniani
7 June 2024, 4:49 pm
picha na Mtandao
Tanzania inapoteza takriban hekta 372,000 za misitu kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni, mkaa, na kilimo.
Ukataji miti umesababisha kupungua kwa eneo la misitu kutoka 45% ya eneo lote la nchi mwaka 1990 hadi 37.7% mwaka 2015 .
Pia Mabadiliko hayo yamesababisha kuongezeka kwa wastani wa joto la dunia
kwa nyuzi joto 1.1°C tangu kipindi cha kabla ya mapinduzi ya viwanda .
Tanzania imekuwa ikikabiliwa na matukio ya hali mbaya ya hewa kama vile
ukame na mafuriko, ambayo yameongezeka kwa kasi katika miongo michache
iliyopita.
Ukame umeathiri zaidi ya watu milioni 14 nchini Tanzania katika miaka 20
iliyopita, na kupelekea kupoteza mazao na mifugo.
Karibu kusikiliza makala hii maalumu kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi, athari zake na juudi za urejeshwaji wa mazingira yaliyoharibika taika wilaya ya Simanjiro kata ya Terrat katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani.