Makala: Fahamu namna shule ilivyonufaika na uhifadhi
27 May 2024, 10:32 am
Na Isack Dickson.
Katika Halmashauri ya Babati, kuna jumla ya shule za msingi 153 ambazo zinahudumia zaidi ya wanafunzi 60,000. Shule ya Msingi Burunge ni mojawapo ya shule mpya zinazokua kwa kasi, ikilinganishwa na shule za zamani ambazo zimekumbana na changamoto za msongamano wa wanafunzi na uhaba wa vifaa vya kufundishia.
Kwa mujibu wa takwimu za elimu mwaka 2023, kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule za msingi za Babati kimeongezeka kwa asilimia 15, kutokana na miradi ya maendeleo inayosaidiwa na jamii na mashirika kama Burunge WMA. Kwa msaada wa Burunge WMA, shule ya Msingi Burunge imeweza kuongeza madarasa manne na nyumba mbili za walimu.
Karibu kusikiliza makala hii maalum kuhusu Namna shule ya Msingi Burunge ilivyonufaika na uhifadhi wa ushoroba wa Kwakuchinja.