Orkonerei FM

Kuzifikia huduma za afya kwenye familia ni jukumu la nani?

23 May 2024, 6:23 pm

Nijuze Radio Show.

Kwa mujibu wa Sera ya afya ya uzazi ya mwaka 2008 inalenga kuboresha afya na ustawi wa wanawake, wanaume na watoto kwa kuzingatia haki za binadamu na uswa wakijisia, sera hii inasisitiza umuhimu wa kuuzuria kilniki kwa pamoja mama na baba wakati wa ujauzito.

Lakini baadhi ya familia hazishirikiani kwenda kliniki kuzifikiia huduma za afya na hii ni kutokana na baadhi ya familia kutoona umuhimu wakuzifikia huduma za afya kwa pamoja,hii ni kutokana na Mila na desturi zinazomfanya mwanamke peke kua na jukumu la kuzifikia huduma za afya.

Katika makala hii ya NIJUZE RADIO SHOW inaangazia ni Jukumu la nani katika familia kuzifikia huduma za afya ? ikiwa na lengo la Jamii kuachana na mila na desturi zinazomfanya mwanamke ndiyo muhusika mkuu wa kuzifikia huduma za afya pamoja na Uwajibikaji wa viongozi kuboresha miundo mbinu ya afya na barabara,karibu kuisikiliza..