Orkonerei FM
Unamwajibisha vipi kiongozi wako kuchukua hatua dhidi ya athari za mafuriko?
10 May 2024, 11:15 am
Nijuze Radio Show.
Kuwepo kwa mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na kuharibu miundombinu,mfano Kwa mwaka 2023 hadi mwanzoni mwa 2024 mafuriko yaliosababishwa na mvua za El Nino yaliathiri miundombinu ya barabara Kwa Wilaya ya Simanjiro.
Lakini Baadhi ya viongozi huwa hawawajibiki ipasavyo kuchukua hatua dhidi ya athari za mvua,kadhalika Baadhi ya Wananchi hawafahamu haki zao za kuwawajibisha viongozi hii inatokana na Ukosefu wa ushirikiano wa jamii na viongozi katika kushughulikia changamoto za mafuriko.
Katika makala hii ya Nijuze wanajamii wametoa maoni yao ya nini kifanyike ili angalau viongozi kushughulikia madhara ya mafuriko ,karibu kuisikiliza.