Wazazi watakiwa kuwasimamia watoto ili kufikia ndoto zao za kielimu.
27 March 2024, 8:01 pm
“Wazazi tunatakiwa tujue mahitaji ya watoto wetu na tuwasaidie kuwatimizia mahitaji hayo kwani wakati mwingine ndiyo yanasababisha wawe watoro.” Mzazi
Na Joyce Elius.
Kikao cha wazazi na uongozi wa shule ya seckondari ya Terrat wilaya simanjiro pamoja uongozi wa kata ya Terrat kimeanzimia kushirikiana kuhakikisha kutatua changamoto zilizopo katika shule hiyo ikiwepo tatizo la upungufu wa madawati 150.
Kikao hicho kilichofanyika leo kimeongozwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Julias Maplani ambaye amebainisha kuwa lengo la kikao hicho cha wazazi ni kujadili changamoto na maendeleo ya shule hiyo.
Naye Diwani wa kata ya Terrat Bw. Jackson Materi akijibu swali la mmoja ya wazazi walioshiriki kikao hicho,amesema njia zitakazo tumika ili kuweza kutatua changamoto ya utoro kwa wanafunzi ni wajibu wa wazazi kuhakikisha mtoto anafika shuleni.
Mratibu wa elimu kata ya Terrat Lucy Urio amewataka wazazi wa wanafunzi 16 wa kidato cha kwanza ambao bado hawaripoti shule kuhakikisha wanafunzi hao wanafika shuleni.
Baadhi ya wazazi walioudhuria kikao hicho wamefurahishwa na wamehaidi kuwa yale yote waliokubaliana kwenye kikao watayafanyia kazi.