Shoroba za wanyamapori Simanjiro zaitesa jamii vijijini
24 February 2024, 12:12 pm
Uwepo wa njia za wanyamapori maarufu kama shoroba kwenye maeneo ya vijijini imekuwa changamoto kwa wananchi kwa kile wanachodai kuwa hawakushirikishwa katika uanzishwaji wake.
Na Baraka David Ole Maika.
Wakizungumza na kipindi cha Uhifadhi na Mazingira cha Orkonerei FM Radio, baadhi wa wananchi wa kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro Jackson Mollel na Stehano Kabuti wamesema kuwa wamekuwa wakisikia uwepo wa mapito ya wanyamapori lakini watu hawafahamu kwa undani na mapito hayo hayatambuliki kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji.
Aidha mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Bw. Kone Peneti Medukenya amesema kuwa utekelezaji wa kanuni za mapito ya wanyamapori hawajawahi kushirikishwa wala kufahamishwa kuwa mapito ya wanyamapori yapo kwenye vijiji vyao.
Naye Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA, Kanda ya Kaskazini Bi. Ruth Philemon anabainisha mkakati wa Wizara ya Maliasili na TAWA wa kuwashirikisha jamii kufahamu na kulinda mapito ya wanyamapori.