Wiki ya maji Simanjiro
15 March 2022, 7:59 pm
HABARI. Na pascal sulle
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 15 Machi 2022 ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet unaogharimu shilingi bilioni 41.5 uliopo Simanjiro mkoani Manyara.
Makamu wa Rais amekagua chanzo cha maji katika eneo la Eltibu na kujionea mtambo wa kusafisha maji katika mradi huo uliopo eneo la loiborsoit.
Akizungumza na wananchi wa Loiborsoit mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo, Makamu wa Rais amewataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kulinda mazingira ili kutopoteza chanzo cha maji kilichopo katika eneo hilo kinachotegemewa katika mradi mkubwa wa maji wa Orkesumet.
Aidha Makamu wa Rais amewaasa wazazi katika eneo hilo kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kutokana na fursa inayotolewa na serikali ya elimu bila malipo pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Katika hatua nyingine ,Makamu wa Rais amewataka viongozi katika ngazi za wizara pamoja na mikoa kuendelea kufanya ziara na kuwafikia wananchi katika maeneo yao ili kutatua changamoto zinazowakabili. Pia amewapongeza wabunge wa mkoa wa manyara kwa ushikirikiano wao katika kuwahudumia wananchi wa mkoa huo.
Kwa uapnde wake waziri wa maji Jumaa Aweso amesema wizara itaendelea kutekeleza miradi kwa ufanisi pamoja na kuokoa gharama zisizo za lazima katika utekelezaji wa mradi hiyo. Waziri aweso amesema utakelezwaji wa mradi huo kwa kutumia wakandarasi wa ndani unatoa fursa ya kuaminiwa kwa wakandarasi wa ndani ya nchi huku akiwataka watendaji katika wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita