Bilioni 1.5 mradi wa maji Terrat Simanjiro
10 March 2022, 7:14 pm
HABARI. na pascal sulle
Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya simanjiro Eng. Johanes Martine amesema serikali imetoa kiasi cha fedha bilioni 1.5 kwa ajili ya kuleta mradi wa maji katika kata ya terat yenye vijiji vitatu na vijiji hivyo vyote vitapata mradi huo.
Akizungumza katika mkutano wa kijiji cha terrat Eng. Johanes Martine amesema tokea siku ya jumanne tumekuwa tukitambulisha mradi huu mkubwa wa maji katika vijiji vitatu ambavyo ni engonongway,nadonjukin na kijiji cha terrat ambapo kwa kila kijiji kina kisima inayozalisha maji mengi na kazi kubwa ni kujenga matenki makubwa katika kila kijiji ili watu waweze kupata huduma hii ya maji.
Amesema mradi huo utatekelezwa kwa miezi sita kuanzia mwezi huu wa tatu na utamalizka kabla ya mwezi wa kumi na tayari mkandarasi atakaefanya hiyo kazi ameshasaini mkataba na kuanzia tarehe 17 na 18 mwezi wa tatu atakabidhiwa majukumu yote kwa ajili ya kuleta vifaa na kuanza kazi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya terrat Jackson Materi ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya raisi samia suluh hasan kwa kutoa fedha ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa maji ndani ya kata ya terrat ambapo kwa mda mrefu vijiji hivyo visima vyake vingi havikuwa vinafanyakazi kutokana na kutokuwa na miundo mbinu ya umeme lakini kwa hivi sasa visima vyote vitafufuliwa kutokana na bajeti kubwa ambayo serikali imeileta katika kata ya terrat.
Mwenyekiti wa kijiji cha terrat bw. Kone Penet Medukenya amesema tumeupokea mradi huu wa maji katika kijiji cha terrat na serikali ya kijiji umeupokea pamoja na wanachi wote kuupokea na kutokana na serikali kusema haitafidia maeneo au miundombinu ambayo yatatumika katika kuupitisha mradi huo wa maji bado koramu kubwa ya wananchi wamekubali miundo mbinu hiyo kupitishwa katika maeneo yao.