Ukeketaji Stop Simanjiro
9 March 2022, 5:30 pm
na pascal sulle simanjiro manyara
Mangariba katika wilaya ya simanjiro mkoa wa manyara wamekubali kuacha kazi ya ukeketaji kwa watoto wa kike ndani ya jamii na kuwashukuru mashirika yote na serikali katika kutoa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji.
Wakizungumza mbele ya katibu tawala wa mkoa wa manyara na mkuu wa wilaya ya simanjiro katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa wa manyara yamefanyika katika wilaya ya simanjiro makao makuu orkesumet.
Wamesema wametambua madhara yanayotokana na ukeketaji ikiwemo kifo lakini pia magojwa mbalimbali ndiyo maana baada ya kupata elimu kutoka kwa mashirika mbalimbali na serikali wakaamua kuachana na kazi hiyo ya ukeketaji na kukabidhi vifaa vya kufanyia ukeketaji kwa mh.katibu tawala ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Katibu tawala wa mkoa wa manyara Bi, Caroline Mtakula amewapongeza mangariba waliojitokeza wenyewe kwa hiari yao na kusema kuwa ukeketaji sasa basi kwani kwa kufanya hivyo wamenusuru maisha ya baadae ya mtoto wa kike kuwa salama .
Sambamba na hilo Mtakula amewaomba wanawake wote kumuunga mkono Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasan katika zoezi la anuani ya makazi linaloendelea nchi nzima kwa hivi sasa na zoezi la sensa linalotarajia kuanza siku za karibuni na kuwaomba watu wote kujitokeza katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.