Orkonerei FM

Recent posts

10 July 2024, 3:27 pm

Migogoro ya ardhi ilivyomnyima kufanya maendeleo

Na Baraka David Ole Maika. Lucas ni mkaazi wa wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha familia yake imekuwa na mgogoro wa ardhi ambao umesababisha kushindwa kufanya maendeleo yoyote katika Ardhi wanayo miliki. Mwanahabari wetu Baraka David Ole Maika amefunga Safari…

9 July 2024, 1:35 pm

Wanajamii wapewa elimu juu ya kujiingizia kipato kipindi cha ukame

Na Joyce Elias. Afisa kilimo kata ya Terrat Ndg.PETRO MEJOOLI LUKUMAY amesema kuwa wanajamii wanatakiwa kulima mbogamboga na mazao mengine mchanganyiko ili kujiingizia kipato haswa wakati wa upungufu wa mvua ama ukame. Ametoa elimu hiyo kupitia mahojiano mafupi aliyoyafanya na…

5 July 2024, 12:02 pm

Migogoro ya ardhi inavyoathiri maendeleo

Kurunzi Maalum Migogoro ya ardhi ni hali ya kutokubaliana au mvutano kati ya pande mbili au zaidi kuhusu umiliki, matumizi, au mipaka ya ardhi. Migogoro hii inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama vile upanuzi wa shughuli za kilimo na ufugaji,…

4 July 2024, 4:26 pm

Umuhimu wa kutumia choo bora

Na Dorcas Charles Wananchi wameshauriwa kutumia choo bora ili kujiepusha na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na magonjwa mengine yanayosbabishwa na uchavuzi wa mazingira Ushauri huo umetolewa na mganga mfawidhi wa kituo cha afya…

4 July 2024, 11:02 am

Unatumiaje ukame kujipatia kipato?

Nijuze Radio Show. Jamii nyingi za kifugaji zinaishi katika maeneo yaliyombali na miundombinu ya umeme, masoko hivyo zinakabiliwa na changamoto za kupata rasilimali na fursa za kuboresha kipato chao kipindi cha ukame,hali inayopelekea kutegemea shughuli moja tu ya kifugaji kujiingizia…

28 June 2024, 11:16 am

Umuhimu wa matumizi ya choo bora

Kwa mujibu wa Ripoti ya Tafiti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya Mwaka 2022 yaani (Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey) imeonesha kuna ongezeko kubwa la watu wanaotumia vyoo bora kutoka asilimia 21…

7 June 2024, 4:49 pm

Maadhimisho ya siku mazingira duniani

picha na Mtandao Tanzania inapoteza takriban hekta 372,000 za misitu kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni, mkaa, na kilimo. Ukataji miti umesababisha kupungua kwa eneo la misitu kutoka 45% ya eneo lote la nchi mwaka 1990…

Dira na Dhamira

DIRA:

Kuwa na jamii ya kifugaji yenye uelewa na ufahamu mpana katika maendeleo kupitia upashanaji wa habari

DHAMIRA:

Kuandaa na kurusha vipindi vya kuboresha maisha ya jamii katika elimu, afya, usawa, uongozi na utawala Bora.

Orkonerei FM Redio ni Redio ya jamii iliyopo katika kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara iliyoanzishwa mwaka 2002 kwa lengo la kuelimisha, Kuhabarisha na kuburudisha jamii za wafugaji na jamii zingine zilizopo katika mkoa wa Manyara,Arusha,Kilimanjaro na mkoa wa Tanga.

Orkonerei FM Redio inapatikana kwa masafa ya 94.3 MHz na kauli mbiu yetu ni “Sauti yako,Sauti ya jamii”