Walinzi wa uhifadhi wanavyohatarisha maisha kulinda shoroba.
30 December 2023, 8:48 am
Juhudi zinazo fanywa na askari wa uhifadhi ,Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wananchi walio jirani katika maeneo ya uhifadhi haswa shoroba ama mapitio ya wanayapori kama Kwakuchinja zinahitajika kuongezwa na kuboreshwa ili kufikia azma kuu ya nchi yetu kufikia watalii milioni 5 na mapato yanayofikia Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.
Na Isack Dickson.
Waziri wa Maliasili na Utalii wa kati huo Mohamed Omary Mchengerwa akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka ya 2023/2024 alisema ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na misitu umeimarika kutokana na juhudi za Serika kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama imefanikiwa kufanya doria 479,242 zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 12,058 pamoja na nyara mbalimbali za Serikali.
Hayo ni matokeo ya juhudi za walinzi wa maliasili hizo lakini yapo madhila chungunzima yanayowakumba wakati wakifanya doria hizo moja wapo ni kuuwawa na majangili wanaofanya uwindaji haramu.Fwatana na mwanahabari wetu Isack Dickson katika makala hii inayoangazia changamoto alizowahi kupitia Bw.JAMES NYASUKA mmoja ya walinzi katika ushoroba wa kwakuchinja.