Orkonerei FM

Malezi ya watoto likizo wazazi watakiwa kuwa makini

6 January 2026, 4:04 pm

Picha kwa maanda wa mtandao

Mwaandishi na Joyce Elias

Wazazi wametakiwa kuzingatia kwa karibu malezi ya watoto wao katika kipindi cha likizo ili kuwalinda dhidi ya kushuka kimasomo na  mmomonyoko wa maadili.

Akizungumza na Orkonerei FM kupitia kipindi cha Mchaka Mchaka Bwana Hassan Fusa amesema kuwa likizo ni kipindi nyeti kinachohitaji uangalizi wa karibu kwa wazazi kwani watoto wengi hukosa ratiba maalum ya kujifunza na kutumia muda mwingi kwenye  michezo, runinga na simu za mikononi.

Aidha amezungumzia changamoto zinazojitokeza kipindi cha likizo ,Bwana Hassan fusa amsema kuwa baadhi ya wazazi huwatwisha watoto majukumu mengi ya nyumbani na kusahu kuwa bado ni wanafunzi wanaitaji muda wa kujisomea na kupumzika

Ameeleza kuwa si vema kwa baadhi ya wazazi kuwapeleka watoto kwenye masomo ya ziada katika kipindi cha likizo akisisitiza kuwa watoto wanahitaji pia muda wa kupumzika ili kuepuka kuchoka kiakili.

Pia ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha uwangalizi unaofaa kwa watoto wote akisisitiza kuwa malezi ya mtoto wa kike na wa kiume ni tofauti na kila moja anaitaji mwangalizi maalumu.