Orkonerei FM
Orkonerei FM
10 November 2025, 8:00 am

Akili mnemba (AI) sasa imeingia kwenye maisha ya kila siku kuanzia vyuoni, biashara hadi mahusiano binafsi, Wengine wanaona ni mkombozi wa elimu na ufanisi, wengine wanaiona kama hatari inayotishia fikra za kibinadamu.
Na Isack Dickson
Kadiri dunia inavyokumbatia teknolojia, matumizi ya akili bandia yamekuwa yakiongezeka miongoni mwa vijana wa vyuo na wafanyabiashara wadogo nchini Tanzania, Wanafunzi wanasema AI imekuwa msaada mkubwa kwenye tafiti na kujifunza, huku wafanyabiashara wakitumia teknolojia hiyo kupanga muda na kusimamia shughuli zao kwa ufanisi.
Lakini pamoja na faida hizo, wataalamu wanaonya kuwa matumizi yasiyo makini yanaweza kuwafanya watu kuwa wavivu kufikiri na kuibua changamoto za upotoshaji wa taarifa. Serikali kupitia sera mpya ya TEHAMA inasisitiza matumizi salama na yenye tija ya akili bandia kwa maendeleo ya elimu na uchumi wa kidijitali.
Sikiliza makala kamili kujua zaidi namna AI inavyobadilisha elimu, biashara na maisha binafsi ya Watanzania. 🎧