Orkonerei FM
Orkonerei FM
23 October 2025, 4:21 pm

Na Evanda Barnaba
Laigwanani Mkuu wa Jamii ya Wamasai, Ndugu Isack Ole Lekisongo, ameongoza uzinduzi rasmi wa shughuli za jando kwa rika jipya la Irmegoliki, ikiashiria mwanzo wa msimu wa 2025-2032 wa sherehe za mila. Sherehe hizo za kihistoria zilifanyika kijiji cha Lengoolwa, Kata ya Lemooti, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Katika hotuba yake kwenye uzinduzi huo, Alaigwanani Isack Ole Lekisongo alisisitiza umuhimu wa kudumisha mila na desturi za Kimaasai katika jami.