Orkonerei FM
Orkonerei FM
1 October 2025, 4:28 pm

Na Isack Dickson
Uchaguzi Mkuu mara zote umekuwa ni moyo wa demokrasia ya Tanzania. Lakini historia imeonyesha kuwa moyo huo mara nyingi unakumbwa na changamoto kubwa—rushwa ya uchaguzi.
Inaanzia ndani ya vyama vya siasa, ambako kura za maoni mara nyingi huchafuka kwa pesa badala ya sera.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupitia taarifa yake ya Mei 2025 ilibaini ongezeko la viashiria vya rushwa, ikiwemo wagombea na wafuasi wao kugawa fedha na zawadi kinyume cha sheria.
Kwenye kampeni, wananchi huchochewa na fulana, kanga, au pesa taslimu, hali inayoathiri maamuzi yao.
Hii ndiyo sura ya rushwa ya uchaguzi Tanzania—inaanzia vyama, inaendelea kwenye kampeni, na kumaliziwa kwenye vyumba vya majumlisho. Lakini licha ya yote, wananchi bado hukumbushwa: “Kura yangu ni haki yangu.”