Orkonerei FM
Orkonerei FM
15 May 2025, 3:03 pm

“Huu ndiyo wakati wa kuhakikisha maeneo yetu ya malisho yanalindwa, kuhifadhi mbegu za majani, na kuhakikisha tunafuata utaratibu wa kulisha mifugo ili kipindi cha ukame kisitukute hatuna maandalizi,” Kone Medukenya
Na Baraka David Ole Maiaka
Jamii ya wafugaji wa kijiji cha Terrat, Wilaya ya Simanjiro, inakumbushwa kutumia vizuri msimu huu wa mvua kuandaa malisho kwa ajili ya mifugo ili kuepuka hasara katika kipindi kijacho cha kiangazi.
Mwaka uliopita wafugaji walipoteza mifugo yao huku wengine wakitumia gharama kubwa kunusuru mifugo kutokana na ukosefu wa malisho na maji. Mfugaji Daniel Leboi Ngoira anakumbusha uzoefu wake katika makala fupi.