Kiongozi wako anawashirikisha vijana katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia?
13 August 2024, 5:47 pm
Nijuze Radio Show,
Kwa mujibu wa Takwimu za Demografia na Afya Tanzania (TDHS) Za mwaka 2015/2016, 40% ya wanawake wenye umri wa miaka 15- 49 wameripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili, 17% wameripoti kufanyiwa ukatili wa kingono.
Katika mkoa wa Manyara, matukio ya ukatili wa kijinsia yameendelea kuwa changamoto kubwa. Takwimu zinaonyesha ongezeko la matukio haya katika miaka ya karibuni. Kwa mfano, taarifa zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Juni 2021, jumla ya watu 15,131 walifanyiwa ukatili wa kijinsia nchini Tanzania, huku matukio mengi yakihusisha wanawake walio katika ndoa.
Karibu kusikiliza makala hii ya nijuze ambayo hukujia kila alhamisi Saa 12:00 jioni na marudio yake ni Jumamosi saa 4:30 Asubuhi.