Kiongozi wako anakabilije athari za kiuchumi zinazoletwa na ukame?
26 July 2024, 11:47 am
Nijuze Radio Show
Kumekuwa na athari za kiuchumi zinazoletwa na ukame katika jamii mara kadhaa wa kadhaa mfano kwa wilaya ya Simanjiro kwa Mujibu wa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Ndg Sendeu Laizer January 13 mwaka 2022 alisema ukame ulisababisha vifo vya mifugo 62,500.
Kwasababu jamii kubwa zinztegemea kilimo na ufugaji kujiingizia kipato hivyo kukiwepo na ukame basi jamii inathirika kiuchumi na baadhi ya Viongozi hawawajibiki ipasavyo kukabiliana na athari za kiuchumi zinazoletwa na ukame.
Katika makala hii ya Nijuze inayokujia kila alhamis saa 12:00 jioni ikiwa na marudio yake Jumanne saa 4:30 asubuhi inaangazia Uwajibikaji wa viongozi katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na Ukame.