Orkonerei FM
Miradi ya maendeleo kata ya Naberera inayotekelezwa na Serikali yafikia patamu.
19 June 2023, 6:30 pm
Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi chungumzima kama vile ya maji,shule na mingine.
Na Isack Dickson
Kata ya Naberera inapatikana katika wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara na ni umbali wa kilomita 146 kutoka Arusha, kwa gari utasafiri kwa saa 2 na nusu kama usipopata usumbufu wowote lakini kutoka Terrat kilomita 52.
Leo Isack Dickson amezungumza kwa njia ya simu na Diwani wa kata hiyo yenye wakaazi 33,344 kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 Bwana Marko Mikael Nunga na swali la kwanza alilomuuliza ni kuhusu miradi inayotekelezwa katika kata yake.