Karagwe FM

Recent posts

29 June 2021, 8:22 am

Agizo kwa waliopata Hati yenye mashaka.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja General Charles Mbuge ameliagiza baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya Karagwe mkoani Kagera kuhakikisha linawachulia hatua za kisheria  watumishi waliobainika kutumia vibaya madaraka ya ofisi na kusababisha Halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka…

29 June 2021, 7:41 am

Wasiojikinga na Covid 19 kukiona cha moto

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi.Julieth Binyula ameziagiza Taasisi za Kiserikali na zisizokuwa za Kiserikali kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa COVI 19. Binyula amesema hayo kupitia mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataka wafanyabiashara pia…

27 May 2021, 8:26 am

Miss Mkoa kukabidhiwa Ndinga ya kisasa.

Mchakato wa Kumpata Mrembo atakayewakilisha Mkoa wa Kagera katika Shindano la Miss Tanzania 2021, umeanza kushika Kasi katika Mkoa wa Kagera, Baada ya Kamati ya Maandalizi kwa kushirikiana na Waandaaji Kutambulisha Rasmi zawadi ya Mshindi wa Taji hilo. Akitambulisha zawadi…

26 May 2021, 8:05 pm

Wapewa mbinu mpya ili kupata Utajiri.

Wanawake wilayani Karagwe wametakiwa kujikumbusha mbinu za masoko ili kuanzisha,kudumisha na kukuza biashara katika ngazi za kikanda na kimataifa. Ameyasema hayo Mke wa Mbunge wa jimbo la Karagwe ambaye ni mkurugenzi wa Alaska Jamii Bi Jeniffar Bashungwa wakati akiongea na…

26 May 2021, 7:07 pm

Wapewa saa 48 kuhamisha vibanda.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Karagwe Godwin Kitonka amewataka wajasiriamali wanaofanya biashara katika stendi ya Kayanga wilaya Karagwe kuhamisha vibanda vilivyojengwa katika eneo hilo kabla ya May 27 mwaka huu. Bwana Kitonka ametoa kauli hiyo Mei 26 mwaka huu…

18 May 2021, 8:59 pm

Watuhumiwa wa wizi wafyekewa Migomba na kubomolewa Nyumba.

Wananachi wenye hasira kali katika kijiji cha Rukole kata Ihanda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wamevamia na kubomoa nyumba pamoja kufyeka migomba ya wananchi wa kitongoji cha Kalalo wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kijijini humo. Akizungumuza katika eneo la…

17 May 2021, 10:16 pm

Watano watumbuliwa Misenyi

Viongozi 5 wa Chama Cha Ushirika wa wakulima wa miwa Missenyi UWAMMISE na BUBARE AMCOS wameondolewa kwenye uongozi baada yakukiuka kanuni na taratibu za Ushirika. Akitangaza kuwaondoa kwenye uongozi Jumatatu Mei 5 mwaka huu ,Afisa Ushirika Wilaya ya Missenyi Gabinus…

12 May 2021, 3:35 pm

Ulinzi kuimarishwa wakati wa Eid.

Jeshi la Polisi wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera  limeanzisha doria maalumu kwaajili ya kupambana na vitendo vya uharifu na kuimarisha usalama wakati wa sikukuu ya Eid EL Fitri. Henry Benard Makwasa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya…

11 May 2021, 12:01 pm

Waziri Bashungwa awafuturisha Waislamu.

Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa ambaye pia ni waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezi amewafuturisha waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wageni waalikwa huku Futari hiyo ikiambatana na harambee ya ujenzi wa kituo cha afya. Shehe wa…

11 May 2021, 11:34 am

Miradi yalamba Milioni 96 kwa miezi 3.

Zaidi ya shilingi Milioni 96 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Kayanga wilaya Karagwe kwa kipindi cha robo ya mwaka 2021. Akizungumza na Redio Karagwe Fm sauti ya wananchi May 11 mwaka huu,Diwani wa kata Kayanga bwana…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171