Orkonerei FM

Ushiriki wa Wananchi Kwenye Mikutano ya Kijamii Kutatua Kero ya Maji

13 December 2024, 3:18 pm

Wakaazi wa lorokare kata ya Oljoro No.5 Wilaya ya Simanjiro wakichota maji katika moja ya korongo la msimu wanalolitegemea kupata maji.

Nijuze Radio Show

Kipindi hiki cha Nijuze Radio Show kutoka Orkonerei FM kinachunguza kwa undani namna ukosefu wa maji unavyowaathiri wakazi wa Kijiji cha Lorokare, hasa wanawake, katika kushiriki mikutano ya kijamii na kufanya maamuzi muhimu ya maendeleo. Mtangazaji Dorcas Charles akiwa studioni, na mwandishi Isack Dickson akiwa moja kwa moja kutoka Lorokare, wanazungumza na wananchi, viongozi wa kijiji, Diwani wa kata, pamoja na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Simanjiro.

Katika kipindi, wanakijiji wanaeleza kwa sauti zao wenyewe jinsi kutafuta maji kunavyowapotezea muda wa kushiriki mikutano, na viongozi wanafafanua hatua zinazochukuliwa kutatua changamoto hiyo. Pia kunapatikana burudani ya mchezo wa redio na ngoma za jadi kutoka kwa jamii ya Maasai.