Keifo FM
Keifo FM
5 October 2026, 2:15 pm

Waandishi wa habari mikoa ya nyanda za juu kusini wametakiwa kujikita zaidi kuandika na kuripoti habari juu ya za watu wenye ulemavu katika mikoa hiyo.
Na James Mwakyeembe
Waandishi wa habari kutoka vituo 10 vya redio nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo ya kuandika na kuripoti habari za watu wenye ulemavu mkoani mbeya.
Mafunzo hayo yametolewa na wawezeshaji kutoka mtandao wa redio za jamii nchini Tadio yakifadhiriwa na wizara ya mambo ya nje ya nchi ya Finland kupitia mfuko wa maendeleo ya vyombo vya habari Vikes kwa siku mbili ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo.
Akizungumza katika mafunzo hayo mhariri mkuu wa jukwaa la habari mtandaoni Hilali Ruhundwa amesema mafunzo hayo yamelenga kuwafanya waandishi wa habari kuandika na kuripoti habari katika maeneo ya vijijini kupitia vituo vyao.
Aidha Ruhundwa ameongeza kuwa wanatarajia kuona vyombo hivyo vya habari vikiendelea kukua na kutumia jukwaa hilo kwa vitendo hasa kwa kupakia habari kupitia teknolojia hiyo mpya pamoja na kuona waandishi wanaendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

Kwa upande wa washiriki kutoka vituo kumi vya redio za jamii nyanda za juu kusini wao wameeleza kuwa mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa hasa katika habari zinazowahusu watu wenye ulemavu.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika jijini Mbeya yakihusisha wandishi ishirini kutoka redio kumi za nyanda za juu kusini yamebeba lengo kuu la kuwaandaa wandishi kuandika na kuripoti habari za watu wenye ulemavu hapa nchini.