Keifo FM

Kyela: Wekeza Group yatoa vifaa vya shule Unyakyusa, Ntebela

3 March 2024, 22:57

Pichani ni baadhi ya wananfunzi wa shule ya Msingi Mbangamojo pamoja na wanakikundi cha Wekeza Grupu wa wa zoezi la kukabidhi vifaa hiyo Na James Mwakyembe

Wakati wanawake wakijiaanda kusherehekea siku ya wananke duniani kikundi cha wekeza grupu kimetoa vifaaa vya shule na chakula kwa shule za msingi Mbangamojo na Ikombe ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya siku ya wananwake hapa wilayani Kyela.

Na Nsangatii Mwakipesile

Kuelekea madhimisho ya siku ya wanawake duniani, kikundi cha Wekeza kilichopo hapa wilayani Kyela kimetembelea na kutoa misaada ya kielimu katika shule ya msingi Mbangamojo iliyopo kata ya Bujonde hapa wilayani Kyela.

Haya yanajiri ikiwa zimebaki siku chache kufikia siku hiyo maalum kwa wanawake ambapo tofauti na ilivyozoeleka kikundi hicho kimeamua kutembelea shule mbalimbali hapa wilayani Kyela ikiwa ni kuhakikisha wanatimiza lengo lao kuwakumbuka watoto katika nyanja ya elimu.

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo vya kielimu mwenyekiti wa  kikundi hicho cha Wekeza amesema wameguswa kufanya hivyo ili kuwatia moyo wanafunzi katika shule za msingi ili waone kuwa wapo wazazi wengine wanaothamini uwepo wao wawapo shuleni.

Sauti ya mwenyekiti Wekeza Grupu Grace Mjengwa akizungumza kuhusu kukabidhi zawadi

Ameongeza kuwa pamoja na kuitembelea shule hiyo lakini kikundi hicho kimepanga kutembelea shule zingine katika kata za Busale, Bondeni tarafa ya Unyakyusa na kisha shule za Mtema zilizopo tarafa ya Ntebela.

Sauti ya Mwenyekiti Grace Mjengwa akieleza kuhusu maeneo watakayo yatembelea.
Pichani wenyekiti wa Kijiji na Kamati ya Shule wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa wekeza Grupu Upendo Mwinuka

Akishukuru kwa niaba ya mwalimu mkuu wa shule ya Mbangamojo mwalimu Zakayo Mtafya amewashukuru wanakikundi hicho na kubainisha kuwa kuwepo kwa maoano yao kuitazama shule hiyo kimewapa faraja tofauti makundi mengine ambayo yamekuwa yakilenga katika maeneo ya mjini pekee.

Sauti  ya Mwalimu Mtafya akishukuru kwa niamab ya mwalimu mkuu wa shule ya Mbangamojo iliyopo kata ya Bujonde hapa wilayani kyela

Kwa upande wa mwenyekiti wa kamati ya shule ya Mbangamojo  Adeni Mwakikalo amesema kitendo hicho kilichofanywa na kikundi cha Wekeza Grupu kuwa ni cha kuigwa wanajamii wengine wanaopenda maendeleo ya kyela.

Sauti ya mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi mbangamojo akishukuru.

Siku ya wanawake duniani huadhishwa tarahe 8 kila mwaka ambayo wanawake husherehekea jinsi wanawake walivyofikia katika jamii,siasa na Uchumi,huku mizizi ya siku hiyo ikimaanisha migomo na maandamano yanayofanywa ili kuongeza uelewa juu ya ukosefu wa usawa unaoendelea.