Keifo FM

Zahanati mpya ya kisasa yanukia Nduka

30 November 2023, 10:42

Mwaenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule Kingamkono kulia kwake ni diwani wa kata ya Ngana Aden Kajela.Picha na Nsangatii Mwakipesile

Baada ya kukosekana kwa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji cha Nduka wilayani Kyela, serikali imepanga kujenga zahanati ya kisasa kijijini hapo.

Na James Mwakyembe

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ambaye ni diwani wa kata ya Ikimba Katule Godfrey Kingamkono amempongeza diwani wa kata ya Ngana na watendaji wa kata ya Ngana kwa kuwarejesha wanafunzi watoro shuleni.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara yake ya kakikazi ya kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Nduka ambayo tangu kuanzishwa kwake hajawai kuwa na miondombinu ya afya.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela Katule Kingamkono akitoa pongezi

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa zanati Katule amewapongeza wananchi wa Nduka kwajitiada zao za kuhakikisha wanapata zanati hambayo inatarajiwa kuwa mkombozi na ustawi bora kwa wakazi wa Nduka hapa wilayani Kyela.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela Katule Kingamkono kuhusu tofali
Picha ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela akiwa na wajumbe wa kijiji na kitongoji cha nduka

Kwa upande wa serikali Katule amesema tayari wamewasiliana na watalamu pamoja na madaktari ili kuangalia uwezekano wa kuanza ujenzi huo mara moja.

Sauti ya Katule Kingamkono kuhusu ujenzi na kuwasiliana na watalamu kuanza usanifu

Kwa upande wa wananchi wamemshukuru mwenyekiti huyo na Diwani wao Aden Kajela kwa kusikia kilio chao na kuaidi kuwa wako tayari kushirikiana na serikali ili kuanza ujenzi huo na kukamilisha mara moja.

Sauti ya wananchi wa nduka wakitoa shukrani mbele ya Serikali

Nduka ni kitongoji kinacho patikana kijiji  cha Ngana  kata ya Ngana Hapa wilayani Kyela ambacho tangu uhuru kimendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mindombinu bora kama barabara, Elimu, Maji, na Afya.