Keifo FM

Kyela:Mwalimu atuhumiwa kubaka mwanafunzi darasa la saba

20 March 2024, 17:27

Picha ya Amina Mapila bibi wa binti aliyebakwa picha na Nsangatii Mwakipesile

Mwalimu mmoja mkazi wa kata ya njisi hapa wilayani kyela anatuhumiwa kumbaka motto mwenye umri wa miaka 14 huku akimuahidi kumuoa na kumpa fedha za kulia shuleni.

Na Nsangatii Mwakipesile

Katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja aliye tambulika kwa jina la Mwalimu Joel mkazi wa kata ya Njisi hapa wilayani kyela mwalimu wa shule moja huko halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe anatuhumiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 14 Mwanafunzi wa Shule ya msingi Njisi Wilayani Kyela.

Huu ni muendelezo wa kutokea matukio ya ukatiri wa kijinsia ambayo yameendelea kuripotiwa sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania ambapo katika siku chache zilizopita mwalimu mmoja huko mara ametuhumiwa kumbaka na kumlawiti wanafunzi anayedaiwa kuwa ni shemeji yake.

Akisimulia kwa masikitiko makubwa Bibi wa motto huyo Amina Mapila ambaye pia ni mlezi wa mototo aliye bakwa jina (linamefaziwa) amesema mnamo tarehe 14 mwezi huu wa tatu ameletewa taarifa kwa wanafunzi wanao soma na mjukuu wake kwamba mwenzao amekuwa akienda fedha shule mara kwa mara hali iliyolazimu bibi huyo kuenda shule na kumhoji mjuu wake mbele ya walimu.

Sauti ya Amina Mapila bibi wa mhanga akisimulia tukio hilo jinsi ilivyolibaini pamoja na hatua alizozichukua

Ameongeza kuwa baada ya vipimo vya kitabibu kukamilika na kuonesha kuwa motto huyo amekuwa akifanyiwa kitendo hicho alirudi kituoni kwaajiri ya mahojiano kisha kurudi nyumbani lakini tofauti na matarajio siku moja baada ya kutoka kituoni mtuhumiwa akarejea nyumbani huku akimnanga bibi huyo

Sauti ya Amina Mapila akieleza juu ya masikitiko yake makubwa ya mtuhumiwa kuachiwa huru bila jambo lake kushughulikiwa

Akiongea kwa ridhaa ya wazazi motto aliyefanyiwa tukio hilo (jina limehifadhiwa)amesema mwalimu huyo alikuwa na mazoea ya kuenda kuchaji simu kisha kumvutia chumbani kwake na kuanza kufanyia kitendo hicho huku akimuambia asimwambie bibi yake na kuwa atampatia fedha za kulia shuleni.

Sauti ya mtoto akisimulia jinsi mwalimu huyo alivyomrubuni kwa fedha na maandazi

Kwa upande wa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaga amesema tukio hilo bado halijafika mezani kwake kwakuwa yeye yuko kwenye majukumu ya kikazi huku akisema atalifuatilia kwa ukaribu kujua namna lilivyoshughulikiwa

Sauti ya ACP Benjamini Kuzaga akizungumzia kuhusu tukio hilo la mtoto kubakwa na mwalimu kyela