Keifo FM

Babylon:  aikacha Chadema atoa mifuko 30 ya saruji  ujenzi wa ofisi ccm

20 September 2023, 10:09

kwenye picha ni Babylon Mwakyambile. picha kutoka maktaba

Babylon Mwakyembile alie Wahi kugombe ubunge kupitia CHADEMA ameamua kuachana na chama Hicho  na kujiunga na chama cha Mapinduzi ambapo katika ujenzi unaoendelea kwenye ofisi ya ccm kata ya Ngusa ametoa vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Na Rahm Sakabona.

Aliye kuwa mwanachama wa cham cha demkorasia na maendeleo chadema Babylon Mwakyembile amekabidhi mifuko 30 ya saruji pamoja na tripu moja ya mchanga na kokoto katika ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi  ccm, kata ya kichama ya ngusa iliyopo kata ya mwaya  wilayani kyela

Babylon amesema amuamua kufanya katika kuhakikisha anaunga mkono njitihada za chama cha mapinduzi pamoja serikali ya awamu ya sita kwa ujumla huku akikili wazi kukihama chama cha  Chadema.

Akikabidhi vifaa hivyo vya ujenzi katika harambee iliyo fanyika katika kata ya kichama ccm ngusa Emmanuel Jotham Aliye kuwa   mwakilishi wa Babylon Mwakyembile amesema kuwa yeye ametumwa  kuwajulisha kuwa kuanzia sasa yeye ni  mwanachama wa ccm na yuko tayari  kushirki shughuli mbalimbali za chama cha mapinduzi.

kulia alie mwakilisha Babylon Mwakyembile Emmanuel Jotham akiteta jambo na mwenyekiti wa ccm kata ya Ngusa
sauti ya jotham babylon amejiunga na ccm

Harambee hiyo pia imehudhuliwa na madiwani mbalimbali wakiongozwa na katibu wa madiwani chama cha mapinduzi Gwakisa Mwakipesile ambaye licha ya kukipongeza chama cha mapinduzi kata ya ngusa lakini pia kama umoja wa madiwani hao  Ambao walifika kwa ajili ya kumuunga mkono diwani wa kata ya mwaya hakimu mwanyilu wamechangia shilingi laki moja.

sauti ya Diwani Gwakisa akiwakilisha umoja wa madiwani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya ngusa  amemshukuru mgeni rasmi kwa mchango alio utoa katika kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo ambapo ameahidi kuanza ujenzi wa ofisi hiyo mara moja na kuwatumia wadau mbalimbali walio ndani ya chama ya mapinduzi ili kukamilisha ujenzi wa ofis hiyo.

sauti ya mwenyekiti ccm kata akishukuru kwa mgeni rasm

Babylon mwakyembile licha ya kuchangia mifuko 30 ya saluji,trip moja za mchanga na kokoto nondo lola tano, lakini pia ameahidi kupeleka tofarai 2000 za kuchoma ili kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo.