Keifo FM

Maadhimisho ya Siku ya Sheria yafana Kyela

2 February 2024, 00:40

Pichani ni wananchi waliojitokeza katika siku ya Sheria hapa wilayani Kyela yaliyofanyika katika viunga vya mahakama ya wilaya Kyela Picha na James Mwakyembe

Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase ameipongeza mahakama ya wilaya ya Kyela kwa kazi ya utoaji haki kwa jamii ya wanakyela kwa ujumla.

Na Nsangatii Mwakipesile

Maadhimisho ya siku ya Sheria hapa nchini Tanzania yamefanyika hapa wilayani Kyela huku ikishuhudiwa mamia ya wananchi wakijitokeza katika mahakama ya wilaya ya Kyela kuungana na mgeni rasmi Josephine Manase mkuu wa wilaya ya Kyela.

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kyela Severin Njau amesema Mahakama hiyo imeweza kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza masuala mbalimbali ya utoaji elimu katika taasisi mbalimbali ikiwemo shule za sekondari,redioni na umma kwa ujumla kupitia vyombo vya habari kama magazeti na redio.

Sauti ya hakimu mkazi mfawidhi Severin Njau akieleza namna mahakama hiyo ilivyoshiriki katika kutoa elimu kwa jamii
Pichani Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kyela akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Kyela wakati akitoa maelezo ya namna mahakama hiyo ilivyofanikiwa katika utoaji haki za kisheria

Ameongeza kuwa katika mwaka uliopita wilaya ya Kyela imesajiri jumla ya mashauri 11 na kumalizika mashauri 17  kwa mahakama ya wilaya pamoja na mashuri mengine sabini na tatu katika mahakama ya mwanzo ambapo mashauri therasini na sita ambapo amesema licha ya mafanikio ipo haja ya kuboresha mifumo ya upatikanaji wa haki kwa lengo la kuleta usawa na ustawi katika jamii.

Sauti ya Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kyela kuhusu uboreshwaji wa mifumo ya haki

Kwa upande wake mgeni rasmi wa wiki ya sheria hapa wilayani Kyela mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amewapongeza mahakimu wote kwa kazi kubwa ya utoaji haki kwa watu wote hapa wilayani Kyela ambapo ametoa ombi kwa mahakama kuhakikisha suala utoaji wa elimu uwe enderevu usio wa kusubiri mwaka hadi mwaka

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase akitoa neno la shukrani mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya ya Kyela wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria
Pichani ni mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase akiwa katika maadhimisho ya siku ya Sheria hapa wilayani Kyela akiwa na katibu tawara wilaya ya Kyela

Miongoni mwa watanzania waliojitokeza wao wamesema wamefurahishwa kuhudhuria maadhimisho hayo ambayo kimsingi wameyataja kuwa fursa muhimu kwao hali ambayo wameitaka jamii ya wanakyela kuwa huru na mahakama ili kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo haki za kisheria.

Sauti ya wananchi waliojitokeza katika siku ya sheria hapa wilayani wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa maazimisho hayo
Picha ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya mahakama wilaya ya Kyela kuadhimisha siku ya sheria hapa nchi Tanzania

Siku ya sheria hapa nchini Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kila kila mwaka kuanzia januari 24 hadi januari 30 ikiashiria kuanza upya kwa mwaka wa mahakama ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika chini ya kauli mbiu ‘umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa taifa nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai’’