Keifo FM

Kyela:CHAMATA Kyela wakiwasha

30 January 2024, 22:07

Pichani ni wajumbe wa CHAMATA wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wakiwa katika kikao kazi cha taasisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Baling’onye Kalebhela Kyela mjini Picha na Nsangatii Mwakipesile

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya CHAMATA Tanzania wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya wameafikiana kuanza kufanya shughuli za utambulisho wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani.

Na James Mwakyembe

Kikao kazi cha kujadiri kuiimarisha CHAMATA wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kimefanyika huku wajumbe wa kikao hicho wakiridhia kwa pamoja juu mambo mbalimbali ya kuimarisha taasisi hiyo mpya ndani ya wilaya ya Kyela.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa Chamata Wilaya ya Kyela Wilium Mwangomile wajumbe wamejadiri hoja mbalimbali zilizolenga kumtangaza na kumsemea Mama Samia Suluhu Hasani Raisi wa jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anazozifanya kwa watanzaia.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi hicho Adamu Mwandali,Upendo Mwandali na George Aldoltego miongoni wa wajumbe wa CHAMATA wilaya ya Kyela wamesema wamekoshwa na kazi kubwa anazoendelea kuzifanya Mama Samia Suluhu Hasani hivyo haoni sababu ya kushindwa kuyasema mazuri mbele ya watanzania wachache wasiojua kuhusu mazuri hayo.

Sauti ya wajumbe wa chamata wilaya ya Kyela mkoa wa mbeya wakizungumza mara baada ya kikao kazi kumalizika
Pichani ni Mwenyekiti Wiliam mwangomile akizungumza mbele ya wajumbe wa kikao kazi.

Kwa upande wa mwenyekiti wa CHAMATA Kyela Wiliam Mwangomile amewashukuru wajumbe kwa kushiriki kikamirifunkatika kikao hicho na kuwaomba watanzania kuhakikisha katika kikao kijacho wanavunja rekodi ya mikoa Mingine pamoja na kutambulisha shughuli mbalimbali za kijamii zinazotaraijiwa kufanyika katika siku chache zijazo.

Sauti ya Mwenyekiti Wiliam mwangomile akizungumza baada ya kumalizika kikao chao leo hii hapa wilayani kyela

CHAMATA ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiriwa na mamlaka husika ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha wanamsemea mazuri anayoyafanya Mama Samia Suluhu Hasani kwa watanzania wachache wasiojua baada ya kuwepo kwa upotoshaji wa baadhi wa wanasiasa wasiopenda maendeleo ya Tanzania ya awamu ya sita chini ya Rais Kipenzi cha watu Samia Suluhu Hasani.

Samia Mitano tena ni lazima