Keifo FM

Wazazi wilayani Kyela wahimizwa kuwapeleka watoto kliniki

11 September 2023, 12:51

Katibu wa watoa huduma kwa watoto wilaya ya Kyela Bakari Samson. Picha na James Mwakyembe

Katika jitihada za kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora, katibu wa watoa huduma za afya kwa watoto wilaya ya Kyela Bakari Samson amewaasa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapelekwa kliniki

Na Secilia Nkili

Imeelezwa kuwa kutompeleka mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano kliniki ni sababu kubwa inayochangia udumavu wa kiafya kwa mtoto kwani mzazi au mlezi atashindwa kufahamu maendeleo ya mtoto wake.

Haya yamesemwa na katibu wa watoa huduma ya afya  kwa jamii wilayani Kyela Bakari Samson wakati wa mahojiano maalum na Keifo FM  ambapo ameeleza kuwa moja ya madhara yanayoweza kumpata mtoto chini ya miaka mitano ni pamoja na utapiamlo jambo linaloathiri afya yake.

Licha ya kubainisha madhara yanayoweza kumpata mtoto ikiwa hatopelekwa kliniki, mtoa huduma huyo amezitaja faida zinazotokana na kitendo cha kumpeleka mtoto kliniki kuwa ni pamoja na  kuepukana na udumavu  na kusaidia kuimarisha afya ya mtoto kwa ujumla…

               

Sauti ya mtoa huduma Bakari Samson

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa watoa huduma wanajitahidi kutoa elimu kwa umma juu ya faida za kuwapeleka watoto kliniki ambapo elimu hiyo imeonekana kuzaa matunda kwa kiasi kikubwa.

                                           

Sauti ya Bakari Samson

Sambamba na hayo amewaasa wazazi wa kiume kuwasaidia wenza wao katika suala la malezi kwa ujumla ikiwemo kumpeleka mtoto kliniki kwani suala la malezi ya mtoto ni la wazazi wote.

                                

Sauti ya Bakari Samson

Tatizo la kutowapeleka watoto walio na umri chini ya miaka mitano kliniki limekuwa gumzo kwa wazazi wengi kwani wengi wao wamekuwa wakikatisha kufanya hivyo kabla umri wa kumpeleka mtoto klinik haijafika  jambo linalohatarisha afya ya watoto wengi hapa nchini.