Kyela:1o8 wakabiziwa vyeti vya udereva Kyela
Keifo FM

108 wakabidhiwa vyeti vya udereva Kyela

6 May 2024, 14:18

Pichani ni Mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya afande H.A Gawile katikati akiwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Kyela Ispecta Seif wakati wa zoezi la kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa udereva kyela picha na James Mwakyembe

Katika kukabiliana na ajali za barabarani jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limetoa vyeti kwa wahitimu miamoja na nane hapa wilayani kyela mbele ya mgeni rasmi afande RTO H.A Gawile.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani H.A Gawile amekabidhi vyeti vya kuhitimu kwa mafunzo ya udereva kwa madereva miamoja na nane hapa wilayani kyela ikiwa ni muendelezo wa jeshi hilo kushirikiana na wadau wengine kuwa na madereva welevu watakao saidia kupunguza wimbi la ajari hapa nchini.

Haya yamejiri katika ukumbi wa kanisa la Romani katoliki hapa wilayani kyela wakati wa shughuli za kuwatunuku vyeti wanafunzi waliohotimu mafuzno ya udereva katika chuo cha        Mj driving school  yakihudhuriwa na mgeni rasmi mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani H.A Gawile.

Akikabidhi vyeti hivyo Mrakibu wa jeshi la polisi kitengo cha usala barabarani H.A.Gawile  amewapongeza wakufunzi wa chuo cha Mj kwa namna walivyojitahidi kuwaandaa madereva hao huku akiwataka wamiliki wa vyuo vingine vya udereva kuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kama hayo kwa waendesha pikipiki maarufu bodaboda.

Sauti ya mrakibu wa jeshi la polisi H.A Gawile kuhusu pongezi kwa chuo na wahitimu kwa ujumla.

H.A.Gawile ameongeza kwa kuwataka wahitimu hao kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti pamoja kufuata sheria zote za usalama  barabarani huku akisisitiza kuwa jeshi hilo litakuwa kali kwa madereva wote wanyekuvunja sheria za usalama wawapo barabarani

Sauti ya gawile kuhusu madereva wenye kuvunja sheria barabarani

Kwa upande wa mkuu wa chuo cha MJ driving school kilichopo Uyole Mbeya Taslo Sanga yeye ametoa shukrani kwa kanisa katoliki hapa wilayani kyela pamoja na jeshi la polisi wilaya ya Kyela chini ya DTO Insecta Seif kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha jambo hilo.

Sauti ya mkuu wa chuo akitoa shukrani kwa jeshi la polisi kyela

Wakizungumza kwa furaha baada ya kupokea vyeti vyao vya uhitimu wa mafunzo ya udereva hapa wilayani Kyela wamemshukuru afande H.A Gawile na chuo cha MJ driving School kilichofanikisha wao kupata vyeti vyao na kuiomba serikali kutilia mkazo chuo hicho kupata wanafunzi wengi zaidi ili kitambulike nchini kote.

Sauti ya wahitimu wa chuo cha Mj driving scool wakitoa shukrani na ombi kwa serikali
Pichani ni wahitimu wa mafunzo ya udereve katika chuo cha MJ driving school wakiwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki wilaya ya Kyela

Mafunzo ya udereva kwa madereva wa vyombo vya moto hapa wilayani Kyela yamehitimishwa kwa kukabidhi vyeti jumla ya madereva miamoja na nane ambao ni madereva wa vyombo mbalimbali vya moto ikiwamo magari ya abiria.