Keifo FM

Kyela:Kishindo maadhisho ya wiki ya jumuiya ya wazazi Kyela Bondeni A yang’ara

4 April 2024, 13:07

Pichani ni wanachama wa chama cha mapinduzi ccm wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondaro Bondeni A picha na Nsangatii Mwakipesile

Wakati chama cha mapinduzi ccm taifa kikiadhimisha wiki ya jumuiya ya wazazi wananchi wilayani kyela wametakiwa kusimamia kikamirifu suala la maadili na kutunza mazingira.

Na Nsangatii Mwakipesile

Maadhimisho ya wiki ya jumuiya ya wazazi wilayani kyela yamefanyika kwa kufanya usafi pamoja na kupanda miti katika shule mpya ya sekondari Bondeni A iliyopo kata ya Bondeni hapa wilayani kyela na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa wa Mbeya Hersi Mwaba.

Akizungumza na kubainisha majukumu yanayofanyika katika kilele cha siku hiyo ya jumuiya ya wazazi hapa wilayani kyela katibu wa jumuiya ya wazazi Kyela Richard Kilumbo amesema majukumu makuu yanayofanywa na jumuiya ni kupanda miti,kufanya usafi katika shule ya sekondari ya Bondeni A,kuendesha kongomano la maadili pamoja na kusajiri wanachama katika mfumo wa kieletroniki.

Sauti ya Richard Kilumbo akizungumzia kazi zinazofanywa na jumuiya hiyo katika sikukuuu hii.
Wanachaa wa chama cha Mapinduzi ccm wilaya ya kyela wakiwa katika zoezi la upandaji miti wakati wa sherehe za wiki ya jumuya ya wazazi wilayani kyela.

Kwa upande wa mgeni rasmi wa maadhimisho ya jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa wa mbeya na mlezi wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela Hersi Mwaba amewataka wazazi kusimamia na kuzingatia kutoa elimu kuhusu suala la mmomonyoko wa maadili ili kuwa na jamii iliyobora.

Sauti ya mgeni rasmi kuhusu maadili kwa watoto hapa wilayani kyela.

Kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira Mwaba amewapongeza jumuiya ya wazazi pamoja na watendaji wa serikali kwa uamuzi huo wa kupanda miti katika shule ya Bondeni A na kuwataka kufanya tendo hilo kuwa la muundelezo shuleni hapo ili kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanakuwa bora na mazuri kwa wanafunzi.

Sauti ya mgeni rasmi kuhusu mazingira
Pichani mgeni rasmi wa hserehe za jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela Hersi Mwaba akipanda mti wake kuashiria zoezi hilo kufanyika kikamirifu

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela Mahamoud Silwamba amewapongeza wanabondeni kwa mwitikio mkubwa waliounesha pamoja na kuwataka wananchi kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kusimamia suala la maadili yaliyomema kwa watoto wa kike na kiume.

Sauti ya mwenyekiti Mahamoud Silwamba kuhusu maadili 44

Maadhimisho ya wiki ya jumuiya ya wazazi kwa wilaya ya Kyela yanafanyika ikiwa ni siku chache kuelekea kilele cha kitaifa ambacho kitafanyika tarehe nane mwezi huu huko jijini Dodoma ambako ndiyo makao makuu ya chama hicho kikongwe barani Afrika.