Keifo FM

Mwankenja: CHADEMA tulieni mambo mazuri yanakuja

11 December 2023, 12:31

Picha ya Mwenyekiti wa uchaguzi kata ya Prospa Mwakilembe akiwa katika ofisi za chama hicho wilayani Kyela

Uchaguzi wa ndani wa chama cha demokrasia na amaendeleo CHADEMA ngazi ya kata ya Kyela mjini umefanyika na kumpata Lafaele Mwankenja kuwa menyekiti.

Na James Mwakyembe.

Zoezi la uchaguzi  wa ndani kuchagua viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA  limendelea hapa wilayani Kyela mkoani Mbeya ambapo Mwenyekiti wa uchaguzi Prospa Mwakilembe washukuru wanachama wa chama hicho kwa utulivu na kufanikisha uchaguzi kwa amani na upendo.

Akizungumza na  mwandishi wa habari Mwakilembe akiwa ofisi za chama cha demokrasia maendeleo CHADEMA zilizopo kata ya Kyela mjini amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo kuanza katika kata hiyo wanachama wamejitokeza kugombea nafasi mbali mbali ambapo hatua za kuwapata viongozi kupitia kata zimefanyika.

Amesema baada ya hutua hizo tayari viongozi wa ngazi ya kata wamepatikana ambao ni Lafaeli Mwankenjaaliyechaguliwa kwa nagazi ya amwenyekiti na katibu wake ni Evance Mwakasege huku katika nafasi ya uenezi aliyechaguliwa ni Timoth Luvanda.

Sauti ya Mwenyekiti wa uchaguzi Prospa mwakilembe

Mshindi wa nafasi ya uenezi kwa ngazi ya kata ya Kyela mjini Timoth Luvanda amewashurukuru wapiga kura wote na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kukieneza chama hicho kwa wananchi wote wa kata ya akyela na wilaya kwa ujumla.

Sauti ya thimos luvanda mshindi wa nafasi ya uenezi kata ya Kyela

Akizungumzia ushindi alioupata mwenyekiti mpya ndani ya kata ya Kyela mjini Lafaele Mwankenja yeye amewashukuru na kuwataka wananchama wa kata hiyo kudumisha mshikamano hasa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuungana katika uchaguzi mkuu ujao.

Sauti ya Mwenyekiti Mwankenja kushukuru

Uchaguzi wa ndani wa chama cha Demokrasi na  Maendeleo CHADEMA unatarajia kuendelea tena kwa ngazi ya wilaya hapo kesho katika kiny’ang’anyiro kinachotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa nafasi ya mwenyekiti wa wilaya ya Kyela.