Keifo FM

‘Cha Malawi’ chateketezwa Kasumulu

23 December 2023, 12:52

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase akiwasha moto juu ya madawa ya kulevya aina ya bangi katika eneo la kijiji cha Ushirika kata ya Ngana wilayani Kyela

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kyela imeteketeza jumla ya tani 154.28 za madawa ya kulevya aina ya bangi zilizokamatwa baada ya misako mbalimbali ya jeshi la polisi wialayni hapa.

Na Nsangatii Mwakipesile

Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kuteketeza kilogramu 154.28 za madawa ya kulevya aina ya bangi zilizokamatwa na jeshi la polisi wilayani hapa kutokana na misako iliyofanywa na jeshi hilo.

Akizungumza akiwa katika zoezi hilo lililofanyika katika kijiji cha Ushirika kata ya Ngana mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase amelipongeza jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama wilaya hapa kwa jitihada hizo kubwa chini ya afande SSP Lwitiko Kibanda OCD wilaya ya Kyela ambazo amezitaja kuwa ni hatua nzuri.

Ameongeza kwa kuwataka wananchi wilayani hapa kuacha kujihusisha na makosa ya kuingiza bangi kinyume cha sharia kwa kujifananisha na nchi jirani ambayo kwao si kosa kufanya kilimo cha bangi na kuitumia.

Sauti ya Mkuu wilaya ya Kyela Josephine Manase kuhusu rai kwa wananchi
Pichani ni Moto mkubwa ukiteketeza madawa ya kulevya aina ya bangi

Kwa upande wa kaimu hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Kyela Paul Barnabas Mabula amepongeza jeshi la Polisi kwa namna ambavyo limeshiriki kikamirifu katika kuhakikisha wanakata madawa hayo ambayo amekiri kuwa kama yangeingia mtaani basi yangeleta adha kwa jamii ususani vijana ambao ndiyo wahanga wakubwa.

Sauti ya Hakimu mkazi mfawidhi akilipongeza jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya usalama

Lwitiko Kibanda yeye ni OCD wilayani hapa amesema zoezi hilo la kuteketeza madawa hayo ya kulevya aina ya bangi limekuja kufuatia jitihada za jeshi la polisi kufanikiwa kukamata na kudhibi madaya hayo kutoka kwa watu walio na nia ovu hivyo kumshukuru mkuu wa wilaya ya Kyela kukubali kushiriki zoezi hilo.

sauti ya SSP Lwitiko Kibanda ocd wilaya ya Kyela

Zoezi hilo la uteketezaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi hapa wilayani kyela linafanyika huku watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara kama hiyo wakiendelea kutorosha kwa njia za panya hasa kutokana wilaya ya Kyela kupakana na chi jirani ya Malawi inayozaniwa kuwa mzarishaji mkubwa wa zao hilo haramu.