Keifo FM

Kyela:Mvua za ng’oa daraja wananchi wapiga mbizi kufuata huduma

4 April 2024, 13:17

Pichani ni Daraj la Mto mwega lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kyesha hapa wilayani kyela picha na Masoud Maulid

Wananchi katika kata ya ngana hapa wilayani kyela wapo hatarini kuliwa na mamba kufuatia  daraja la mto mwega kubomoka na kulazimika kuvuka kwa kuogelea ndani ya mto huo unaosifika kuwa na mamba wengi kufuata huduma kijiji cha pili.

Na Masoud Maulid

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa wilayani kyela na kusababisha adha kubwa wananchi wa kijiji cha Ushirika Kata ya Ngana Wilaya ya Kyela wameiomba Serikali kufanya mchakato wa haraka ili kurudisha mawasilino ya barabara baada ya daraja la mto mwega kukatika.

Wakizungumza na Mwandishi wa Habari wananchi hao wamesema,kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zimepelekea mto mwega kufurika na daraja la mto huo kukatika hivyo kukosekana mawasiliano kati ya wananchi kutoka kitongoji kimoja kwenda vitongoji vingine,hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu kuenda kijiji cha Ngana kwa ajili ya mahitaji mbalimbali.

Sauti ya wananchi  kuhusu daraja kukatika na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ushirika Juma Kashililika pamoja na Mwalimu wa shule hiyo Patrick John  wamesema,kukatika kwa daraja hilo ni pigo kubwa kwa wananfunzi wanaosoma shule hiyo  na wanafunzi wengine wanaotoka vitongoji jirani  kwenda shule ya sekondari masukila,ambapo kwa sasa hawawezi kupita katika eneo hilo jambo ambalo linatishia uhakika wa elimu yao.

Sauti ya  Juma kashililika kuhusu wanafunzi kushindwa kufika shule kutokana na daraja hilo kukatika
Pichani ni barabara ikionesha athari jinsi zilivyokubwa kwa wakaazi wa ngana baada ya kukatika kwa daraja wa mto mwega

Nae afisa mtendaji wa kijiji hicho Andendekisye Mwakalinga amesema,kukatika kwa daraja hilo mbali ya kuwa ni  changamoto kwa wanafunzi na walimu kushindwa kufika shuleni,pia eneo hilo  ni changamoto hata kwa wananchi kuvuka eneo hilo kwenda  kwenye shughuli za kilimo,hivyo inalazimika kuvuka kwa kuogelea wakati wa kwenda na kurudi hali ambayo ni hatari kwa maisha yao

Sauti ya  afisa mtendaji kuhusu wananchi kuwa katika hatari ya kupoeza maisha kutokana na kuvuka eneo hilo kwa kuogelea

Diwani wa kata ya Ngana Aden Kajela amewataka wananchi kuchukua tahadhari wanapovuka eneo hilo kwa kuogelea kwani madhara yake ni makubwa kutokana na mto huo kuwa na mamba na kuongeza kuwa,kwa kushirikiana na afisa mtendaji wa kata wameandika barua kwa ajili ya kumjulisha meneja wa tarura,katibu tarafa,pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri na tayari meneja wa tarura ameahidi kufika eneo hilo.

Sauti ya diwani wa kata ya ngana Aden Kajela akizungumza kuhusu hatua zilizochukuliwa

Daraja la mto mwega ni kiunganishi baina ya vitongoji vya makaso na lusungo kwa upande ilipojengwa shule ya msingi, huku vitongoji vingine vilivyo kwenye kijiji hicho ni maparakata,ibungubati na kasyunguti vyote vikiwa kijiji cha ushirika kata ya ngana.