Keifo FM

Kyela:Vitambulisho 36 elfu vya utaifa vyatolewa na NIDA Kyela

11 January 2024, 17:42

Pichani ni afisa wa uandikishaji wilaya ya Kyela Kenan Kamwela Picha na Nsangatii Mwakipesile

Baada ya serikali kutoa vitambulisho vya utaifa vya NIDA kwa wilaya ya Kyela wananchi wilayani hapa wamesusia kuchukua vitambulisho hivyo licha ya serikali kutumia nguvu kubwa katika kuwahamasisha.

Na James Mwakyembe

Siku chache baada ya mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase kutangaza kupokea jumla ya vitambulisho vya Taifa NIDA elfu arobaini na tano wito umetolewa kwa wananchi wilayani hapa kuchua vitambulisho vyao katika ofisi za kata zinapatikana katika maeneo yao.

Kauli hiyo inakuja kufuatia mrundikano wa vitambulisho hivyo katika baadhi ya ofisi za kata kutokana na wananchi wengi kutofika kuvichukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa na serikali desemba mwaka jana.

Akizungumza na keifo fm afisa msajiri wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA wilaya ya Kyela Kenani Kamwela amesema serikali imetoa jumla ya vitambulisho elfu arobaini na tano kwa wilaya ya kyela ambapo mpaka sasa jumla ya vitambulisho elfu therathini na sita sawa na asilimia 81.

Sauti ya Kenan Kamwela akizungumzia idadi ya vitambulisho vilivyopokelewa na kugawaiwa kwa wananchi

Kamwela amesema changamoto kubwa alijitokeza ni wananchi wengi kutokujua umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa hali inayowapelekea kujikita zaidi katika majukumu yao ya kifamilia licha ya serikali kutoa matangazo katika vyombo vya habari na taasisi za kidini.

Pichani afisa mwandikishaiji wilaya ya Kyela Kenani Kamwela akiwa katika ofisi za mamlaka hiyo wilayani Kyela

Aidha ameongeza kuwa njia mbalimbali zimetumika katika kuwahamashisha wananchi li kujua na kuvichukua vitambulisho vyao kabla ya serikali kuvichukua tena na kuvirejesha katika mamlaka hiyo hapa wilayani kyela.

Sauti ya Kenani Kamwela akizungumzia njia zilizotumika kuhamisisha wananchi

Keifo fm imefanya mazungumzo na baadhi ya wananchi wilayani hapa kujua kama je wanatambua kama vitambulisho vya utaifa vimekwisha kufika?na Je ni hatua zipi wamezichukua ili kuvichukua vitambulisho hivyo?

Sauti ya baadhi ya wananchi walioulizwa na Keifo fm kuhusu uchukuaji wa vitambulisho vya utaifa vya NIDA

Kwa upande wa Daniel Mashaka mkazi wa wilaya ya kyela ambaye nimiongoni mwa wananchi waliochukua vitambulisho mapema kabisa yeye ameeleza kuwa muitikio mdogo wa wananchi katika kuchukua vitambulisho hivyo unatokana na wao kutokujua umuhimu wa vitambulisho vya taifa katika kazi zao za kila siku.

Sauti ya Daniel Mashaka mkazi wa kyela waliochukua vitambulisho mapema akieleza kuhusu umuhimu wa vitambulisho

Mwezi disemba mwaka 2023 wilaya ya Kyela imepokea jumla ya vitambulisho elfu arobaini na tano kutoka mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ambavyo vimesambazwa katika ofisi mbalimbali za kata hapa wilayani Kyela ili wananchi waweze kuvichukua lakini tofauti na matarajio ya serikali vitambulisho hivyo vimeendelea kusalia katika ofisi hizo.