Keifo FM

Kyela: Ngedere watishia janga la njaa Ipande

11 December 2023, 12:42

Pichani ni diwani wa kata ya Ipande Stevini Mwangalaba Picha na James Mwakyembe

Wanyama waharibifu kwa mazao ya chakula aina ya Ngedere wamevamia mashamba ya wananchi wa Ipande na kula mazao shambani.

Na Nsangatii Mwakipesile

Kufuatia kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazao unaofanywa na wanyama aina ya ngedere wakulima wa Kata ya Ipande Wilayani Kyela wameitaka serikali kupitia afisa mazingira wa halmashsuri ya wilaya ya Kyela kushughulikia tatizo hilo linalotishia jamii hiyo kukumbwa na njaa.

Wakizungumza kutoka kijijini hapo wamesema wanyama hao wamekua ni kero kwao kutokana na uvamizi hali inayo watia hofu ya kukumbwa na njaa.

Sauti ya wananchi wa Ipande wakiomba msaada kwa serikali

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mbula Alfred Mwalikuta amesema wamekuwa wakipambana na wanyama hao waharibifu kwa njia za asiri kitu ambacho kimewapa ugumu wa kuondokana na tatizo hilo hivyo kumtaka afisa wa mazingira kuingilia kati.

Sauti wa Mwenyekiti wa kitongoji cha mbula akizungumzia namna wanavyokabiriana na byani hao

Kwa upande wa diwani wa kata ya Ipande ambaye ndiye muwakilishi wa wananchi kwa ngazi ya halmashauri Stivini Mwangalaba amesema tayari jambo hilo amelifikisha halmashauri ya wilaya ya Kyela licha ya kukiri kuwa kwasasa mtalaamu amehamishiwa kituo kingine.

Sauti ya diwani wa kata ipande akizungumzia kuhusu kadhia ya ngedele

Kutokana na hali hiyo Mwangalaba amewaomba wananchi wake kuendelea kupambana na wanayama hao haribifu kwa mazao yao kwa kutumia njia za asiri wakati serikali ikilitafutia suluhu jambo hilo.

Amemaliza kwa kuwataka wananchi wa kata ya Ipande kuendelea kujiandaa na msimu mpya wa kilimo hasa kwa kuhakikisha wanazitumia mvua hizi vizuri ili kuondokana na kitisho cha njaa kinachosababishwa na mabadiriko ya tabia nchi.